Lishe bora kwa mtoto mchanga ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wake. Baada ya kuzaliwa, mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama. Kwa kifupi, hakuna chakula mbadala kwa ambacho kina virutubisho vya kutosha na bora kwa mtoto mchanga kama maziwa ya mama.
Baada ya kujifungua, mama hutoa maziwa mepesi ya rangi ya njano (colostrum), maziwa haya huwa na virutubisho muhimu na kinga za mwili ambazo humsaidia mtoto katika ukuaji.
Maziwa ya mama yana vitu vifuatavyo;
- Wanga aina ya lactose
- Mafuta
- Protini aina ya casein, albumin na lactoferrin hufanya sehemu kubwa ya protini zilizo katika maziwa.
- Vitamini
- Madini ya kalsiam, sodiamu, potasiamu , klorini na fosforasi.
- Protini za Kinga ya mwili ambazo husaidia kuimarisha kinga ya mtoto.
Kwa kifupi, hakuna chakula mbadala kwa ambacho kina virutubisho vya kutosha na bora kwa kichanga kama maziwa ya mama. Kumnyonyesha mtoto wako ni uamuzi mzuri sana kwa ajili ya afya yake.Mtoto mchanga wa chini ya miezi 6 anatakiwa anyonyeshwe maziwa ya mama pekee hadi atakapofikisha miezi 6.
Mambo ya Kuzingatia;
Nyonyesha mara nyingi kadri mtoto anavyohitajii wakati wote, usiku au mchana. Unaweza ukamnyonyesha mara 8 mpaka 14 ndani ya masaa 24 au kila baada ya masaa 2 mpaka 3.
Nyonyesha mara nyingi kadri mtoto anavyohitajii wakati wote, usiku au mchana. Unaweza ukamnyonyesha mara 8 mpaka 14 ndani ya masaa 24 au kila baada ya masaa 2 mpaka 3.
Mnyonyeshe anapoonesha dalili za njaa kama kuhangaika, kulia, kunyonya vidole au midomo.
Hakikisha mtoto ananyonya ziwa moja mpaka liwe laini au maziwa yaishe, kisha umuhamishie kwenye ziwa lingine.
Usimpe chakula au vinywaji vingine. Maziwa ya mama ni lishe tosha kwa mtoto chini ya miezi 6!
No comments:
Post a Comment