KATIKA hali isiyo ya kawaida, askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Mkoani Mtwara jana walisimamisha vyombo vya usafiri barabarani asubuhi na kushusha abiria waliokuwemo, ili washiriki kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi.
Ufanyaji usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi umekosa mwamko mjini Mtwara tangu kuzinduliwa na Rais Desemba 9, mwaka jana.
Bila kujali itikadi za vyama wala cheo cha mtu, JWTZ waliwataka wananchi kupaki vyombo vya usafiri na kufanya usafi ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa.
Baadhi ya wananchi walioshiriki usafi huo, walipongeza jitihada za JWTZ katika kutilia mkazo zoezi la usafi mkoani humo.
Sefu Mponela alisema kuwa sehemu yoyote yenye watu wastaarabu ni lazima wawe wasafi, na kuomba wananchi kuendeleza hali hiyo iliyohamasishwa na JWTZ ili kupambana na magonjwa ya milipuko mkoani humo.
“Ni jambo la kupongeza sana, hasa Mkuu wetu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya kwa kuendeleza usafi mkoani kwetu," alisema Mponela.
"Askari polisi, wanajeshi, mama lishe na hata viongozi mbalimbali naona wanashiriki hapa. Nimefarijika na hakika Manispaa yetu itakuwa safi ikiwa tutaendeleza jambo hili.”
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Mohamed Sinani alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kufanya usafi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa ya milipuko.
“Sisi kama viongozi wa siasa tujenge tabia ya kuwahamasisha wananchi wetu," alisema Sinani.
"Lazima kila mtu afanye usafi bila kujali chaama, magonjwa ya mlipuko yanapotekea hayachagui chama kila mtu ataadhirika ni lazima tujenge tabia hii ya kufanya usafi.”
Zoezi hilo la usafi liliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego ambaye alisema litakuwa endelevu mkoni hapo.
NIPASHE.

No comments:
Post a Comment