Thursday, 5 May 2016

BEI YA SUKARI YAPAA HADI SH 3000 KWA KILO



WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro, wamelalamikia wafanyabiashara wa maduka madogo kutokana na kupandisha bei ya sukari na kuuzwa Sh. 3,000 kwa kilo.




Wakizungumza na wanahabari, baadhi ya wananchi hao walisema bei hiyo imepanda ghafla kutoka Sh. 1,900 hadi Sh. 3,000 baada ya serikali kutangaza upungufu wa sukari nchini.
Hata hivyo, wafanyabiashara wa maduka wamewatupia lawama mawakala wakubwa wa sukari kutokana na kuwapandishia bei wafanyabiashara hao kwa kuwauzia mfuko wa kilo 25 kwa Sh. 65,000 na mfuko wa kilo 50 kwa Sh. 120,000.
Mmoja wa wafanyabiashara wa duka katika Kata ya Uwanja wa Taifa, Said Omary, alisema wamekuwa wakipokea lawama na malalamiko kutoka kwa wananchi kufuatia mfumuko wa bei ya sukari.
“Nikweli tunapokea lawama nyingi kutoka kwa wateja wetu, lakini ndio hali halisi kutokana na manunuzi yetu kutoka katika maduka ya jumla,” alisema Said Omar.
Aidha, mmoja wa wananchi hao, Omary Salum, alisema serikali inapaswa kuliangalia suala la mfumuko wa bei ya sukari kutokana hali duni za wananchi.
“Sukari imepanda kutoka Sh. 2,200 mpaka Sh. 3,000 hali ambayo kwa sasa dalili za wananchi kuanza kunywa uji wa chumvi kurudi tena,” alisema.
Chama cha kutetea maslahi ya wakulima wa miwa katika Bonde la Kilombero (KCGA), kimedai kusimamia suala la makubaliano na kiwanda cha sukari cha Illovo na kupandisha bei ya miwa kwa tani kutoka Sh. 72,799 hadi Sh. 79,620 Mwenyekiti wa KCGA, Novatus Mwananengule, alisema katika mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kueleza malipo ya utamu wa sukari katika miwa (landment) yamepanda kutoka asilimia 9.08 hadi 10.49 na yote hayo yatalipwa.
NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!