Sunday, 1 May 2016

ASHINDA KESI YA KUBAKA MTOTO



MAHAKAMA ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imemwachia huru mtuhumiwa wa kosa la ubakaji wa mtoto wa miaka 13, Mmanga Hamdani (47)




Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfadhi Mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Tunduru, Gladys Barthy alisema amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na mganga wa hospitali ya wilaya ya Tunduru, Dk. Gaofridi Mvile kuwa mtoto huyo hakubakwa.
Akifafanua hukumu hiyo, Hakimu huyo alisema mahakama imeamua kutenda haki kwa kutoa uamuzi huo wa kumwachilia huru kwa sababu huenda binti huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita, alimsingizia mthumiwa huyo ambaye ni mjomba wake kwa lengo la kutaka kumkomoa.
Akinukuu taarifa ya ushahidi uliotolewa na daktari huyo, Hakimu huyo alisema siku ambayo mlalamikaji alifanyiwa vipimo vya ukaguzi wa kuthibitisha tukio la ubakaji, hakuonyesha kuwa na dalili za kuingiliwa.
Alisema vipimo vilionyesha kuwa msichana huyo bado ana bikra yake na kwamba kilichobainika katika uchunguzi huo ni kuwepo kwa mrundikano wa damu ambazo zilitolewa kwa kumfanyia upasuaji wa tumbo lake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na tabia ya kumuingilia kimapenzi mwanafunzi huyo wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Nanjoka, na kwamba pia alikuwa akimuingilia kinyume cha maumbile katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwendesha Mashtaka Inspekta wa Polisi, Songelaeli Jwagu alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hiyo Februari 21, mwaka huu majira ya saa 4.40 usiku baada ya kumvamia na kumziba mdomo mtoto huyo na kufanikisha adhima yake hiyo.
Katika utetezi, Mmanga alipeleka mashahidi watatu lakini daktari huyo ambaye alipelekwa na upande wa Jamuhuri kati ya mashahidi wao watano, alisaidia kumpa haki mtuhumiwa bila kuacha shaka.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!