Friday 6 May 2016

AKAMATWA AKITISHIA KUWAPIGA BASTOLA WACHIMBAJI WADOGO


JESHI la polisi wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, linamshikilia Nyambaria Karigita, kwa kosa la kuwatishia kuwaua kwa bastola wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi uliopo kijiji hapo.



Karigita ambaye anamiliki leseni ya uchimbaji wa madini, alidaiwa kuwanyang’anya na kuwafukuza katika machimbo hayo wachimbaji hao ambao walikubaliana watakuwa wanachimba dhahabu na kumpatia asilimia nne kati ya 10 wakati wa uzalishaji wa madini hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’azi, alithibitisha kukamatwa kwa mtu huyo na kuahidi upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Wakizungumza na Nipashe juzi, baadhi ya wachimbaji waliopo katika mgodi huo, walilalamikia kitendo cha kunyang’anywa shimo hilo la kuchimba dhahabu na mfanyabiashara huyo na kuwatishia kuwaua kwa kuwapiga risasi.
Baraka Leonard, ambaye ni mmoja wa wachimbaji hao, alifika ofisi za kijiji hicho na kuonana na Ofisa mtendaji, Elisha Henry, ili mlalamikaji huyo aende vyombo vya sheria kulalamikia hali hiyo.
Makamu mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wilayani humo, George Miyawa, alishangazwa na vitendo vya mtu huyo na kukemea hali hiyo na kuviomba vyombo vya serikali kufuatilia.
Kufuatia tukio hilo, wachimbaji hao walifungua kesi polisi ya kutishia kuua.
NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!