Wachimbaji wadogo wawili katika mgodi wa dhahabu uliopo kijiji cha Mangae wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamefariki dunia baada ya shimo walilokuwa wakichimba kujaa maji kufuatia mvua zinazoendela kunyesha mkoani humo.
ITV imfika katika machimbo hayo majira ya saa mbili usiku nakukuta wananchi wakitumia mwanga wa tochi na jenereta kuvuta maji kwenye mgodi ili kuitafuta miili hiyo ambapo kwa upande wao mashughuda waliokuwepo na marehemu hao ameeleza jinsi ilivyo tokea.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Berege Alex amesema walipopata taarifa ya kutokea janga hilo walikimbia kwenda kutoa msaada huku wakiwasiliana na viongozi wa kata na polisi kupata msaada wa kuwaokoa.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Urich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mgodi huo uliozuiliwa miaka mitatu iliyopita na kuwataka wananchi kuacha kujishughulisha na shughuli za uchimbaji madini kipidi hiki cha mvua.
No comments:
Post a Comment