Wednesday 13 April 2016

TASWIRA MSIBA WA NDANDA KOSOVO

Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) samabamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda wakiwa msibani hapo.





Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Ndanda Kosovo, King Dodoo akiweka mambo sawa msibani.



King Blaise wa  FM Academia akiimba kwa huzuni.

Mama  yake  Ndanda Anne  Mariane Kombe akilia kwa uchungu.

Mke  wa pili wa  marehenu, Infrancie.



Francie  akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe.




Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu.



Totoo Zebingwa  akimsalimia  


WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar,
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanamuziki huyo, King Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!