Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) imetahadharisha uwepo wa mvua kubwa na upepo mkali unaozidi kasi ya km 40 kwa saa kuanzia Aprili 26 hadi Aprili 28 mwaka huu.
Sambamba na upepo huo zinatarajiwa kunyesha mvua za zaidi ya milimita 50 huku bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0
Hali hiyo inakuja kufuatia kuwepo kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika pwani ya Tanzania unaotakana na kimbunga cha Fantala.
Kwa mujibu wa TMA maeneo yanayotarajiwakuathirika ni mikoa ya Tanga,Dar es Salaam,Morogoro,Lindi,Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mvua hizo pia zinatarajiwa kusambaa katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro na Mashariki mwa Manyara
No comments:
Post a Comment