Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imetangaza kuwa kuanzia leo itazifunga kwa muda shule zote za awali, msingi na sekondari katika mkoa wa Mjini Magharibi, ambazo ziko kwenye maeneo yaliyokumbwa na hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, hatua hioyo inatokana na kuwapo kwa habari za kulazwa baadhi ya wanafunzi katika kambi za kipindupindu na wengine kufariki dunia.
Waziri na Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, katika taarifa yake hiyo jana alisema serikali imechukua hatua hiyo baada ya kufanya tathmini na kuona kuwa baadhi ya shule zimeathirika, baada ya kuingiliwa na maji ya mvua zilizonyesha hivyo kuhatarisha usalama wa walimu na wanafunzi.
Miongoni mwa shule zilizotangazwa kufungwa kwa upande wa shule za msingi ni Welezo, Urafiki Mwanakwerekwe, Chunga, Kilimahewa, Chumbuni, Mtoni Kidatu, Dimani, Koani, Kitogani, Pangatupu na Kokota.
Kwa upande wa shule za sekondari ni Bwefum, Langoni, Uzi na Pete.
Aidha, waziri huyo aliwataka wananchi kuchukuwa tahadhari kutokana na kipindupindu kushika kasi Zanzibar na kusababisha vifo vya watu wengi.
Hata hivyo, maeno yote ya Zanzibar, biashara za vyakalu ikiwamo mama ntilie na viosiki mbalimbali vimefungwa hadi maradhi ya kipindupindu yatakapoisha.
Kipindupindu Zanzibar kimedumu kwa miezi saba sasa tangu Septemba, mwaka jana na kusababisha zaidi ya watu 40 kufariki dunia na wengine zaidi ya 3,000 kuugua maradhi hayo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, hali ya ugonjwa huo kwa sasa ni ya kutisha na kambi ya kipindupindu iliyoko Chumbuni, wilaya ya Magharibi Unguja inapokea wastani wa wagonjwa 40 kwa siku.
Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo, alisema kuwa chanzo cha kuongezeka kwa maradhi hayo ni uchafu uliokithiri na mvua kubwa zinazonyesha Zanzibar, ambazo zimesababisha mafuriko.

No comments:
Post a Comment