Thursday, 28 April 2016

POLISI MOROGORO WAFUNDISHWA KICHINA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest

Morogoro. Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM), limeanza kutoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa askari ili kurahisisha mawasiliano baina yao na raia wa China.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa wanafunzi hao, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Betha Matiku amesema Wachina wanapofanya ama kufanyiwa vitendo vya uhalifu, jeshi hilo limekuwa likitafuta wakalimani wa kutafsiri na hali hiyo inaweza kuharibu upelelezi wa kesi.
Betha amesema hivi sasa ni wiki ya tatu tangu waanze mafunzo hayo ya miezi mitatu, lakini tayari wameanza kuelewa mambo muhimu ambayo yatawasaidia katika kutoa huduma kwa raia hao.
“Wachina sasa hivi wameonekana kuingia kwa wingi hapa nchini, hivyo lazima tuijue lugha hii ambayo itatusaidia katika kutoa huduma kwao. Mara nyingi tumekuwa tukipata tabu kuwasiliana nao, kwani wengi wao hawajui Kiingereza, hivyo tunalazimika kutafuta wakalimani,”amesema.
Ofisa Habari wa jeshi hilo Mkoa wa Morogoro, Badru Mtambo amesema mafunzo hayo yanatolewa na mhadhiri kutoka MUM ambaye ni raia ya China, Sun Xlaofel.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!