Saturday 16 April 2016

Papa Francis arejea na wahamiaji Vatican

PapaImage copyrightReuters
Image captionWahamiaji wakielekea kuabiri ndege iliyombeba Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewachukua wahamiaji 12 kutoka Syria na kwenda nao Vatican baada yake kutembelea wahamiaji katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki.


Wahamiaji hao kutoka familia tatu wote ni Waislamu, na miongoni mwao kuna watoto sita.
Nyumba za familia hizo zilishambuliwa kwa mabomu wakati wa vita nchini Syria.
Vatican imesema kupitia taarifa kwamba Papa Francis amechukua hatua hiyo kuwaonesha wahamiaji kwamba wanakaribishwa.
Maelfu ya wahamiaji kwa sasa wamekwama katika kisiwa cha Lesbos kufuatia mkataba wa mwezi jana kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki ambao unalenga kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Wahamiaji wote walioondoka na Papa walikuwa tayari wanaishi Lesbos kabla ya mkataba huo kuanza kutekelezwa, Vatican imesema.
Chini ya mwafaka huo baina ya EU na Uturuki, wahamiaji wanaofika kwa njia haramu katika visiwa vya Ugiriki kutoka Uturuki baada ya tarehe 20 Machi watakuwa wakirejeshwa Uturuki iwapo hawatafanikiwa kuomba hifadhi.
Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU itampokea mhamiaji mwingine kutoka Syria aliyeko nchini Uturuki.
Awali, Papa Francis aliambia wahamiaji wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Moria, baadhi wakikabiliwa na uwezekano wa kurejeshwa Uturuki, kwamba "hamjaachwa peke”.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!