Saturday, 30 April 2016

MTUMISHI WA TANESCO AKIOMBA RUSHWA "AMEKWISHA"


MKURUGENZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Injinia Felchesmi Mramba, ameagiza apelekewe taarifa ya mtumishi yeyote atakayeomba rushwa kabla na baada ya kutoa huduma kwa wananchi.



Amesema atafikisha taarifa hizo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na akithibitika atashughulikiwa ikiwamo kufukuzwa kazi na kushtakiwa.
Aidha, alisema wananchi kupata huduma za Tanesco kutoka kwa watumishi wa shirika hilo ni haki yao na kwamba mtanzania yeyote atakayeombwa rushwa atoe taarifa haraka.
Mramba alitoa kauli hiyo wakati akizindua mfumo wa majaribio wa ‘Tanesco Huduma’ utakaowarahisishia wananchi kuwasilisha kero mbalimbali kwa njia ya mtandao kupitia simu zao za mkononi.
Alisema wananchi wengi wanalalamika kwamba hawapati laini ya simu kutokana na kuwa muda wote zinatumika.
Alisema shirika lake limeanzisha huduma hiyo kwa majaribio na itaanzia Mkoa wa Kinondoni Kaskazini na baadaye njia hiyo ikionyesha mafanikio itaunganishwa kwa wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam.

Akifafanua kuhusu mfumo huo kupitia mtandao pekee, Mramba alisema kwa wale wasiokuwa na simu za viganjani wataunganishwa kwa njia ya ujumbe mfupi ili kufanikisha upatikanaji wa huduma bora.
Naye mtaalam wa mfumo huo, Godfrey Magila kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), alisema mfumo huo utatumia simu za smatphone na kwamba watumiaji watajiunga kama mitandao mingine ya kijamii kutuma na kupata taarifa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!