Monday 11 April 2016

MTUHUMIWA WA WIZI WA BODABODA AKAMATWA TANDALA-MAKETE


Kijana Eliud Kasimiri (19) mkazi wa Lyamkena Makambako mkoani Njombe amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa pikipiki yenye namba za usajili MC 282 AQG mali ya Edga Mbilinyi mkazi wa mtaa wa posta kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe.



Mtuhumiwa huyo amekamatwa jana alfajiri kwa ushirikiano na madereva bodaboda wa kata ya Tandala akiwa anajaribu kutoroka na pikipiki hiyo katika kijiji cha Mgodechi wilayani Njombe na kufanikiwa kumfikisha katika kituo cha polisi Tandala kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Alipo hojiwa na jeshi la polisi mtuhumiwa huyo amesema kuwa alitumwa na mkazi mmoja wa Njombe ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa Huku akizungumzia na uwepo wa gari la wizi uliofanywa na aliyemtuma.
Akizungumza na blog hii mmoja wa viongozi wa bodaboda Tandala Bw. Federiko Mahenge amesema kuwa wizi huo umekuwa ukijitokeza mara kwa mara kwa zaidi ya miaka minne sasa na zaidi ya pikipiki sita zimeibiwa huku akiongeza kuwa huwenda kuna mwenyeji anayeshirikiana na wezi hao.





Mpaka sasa mtuhumiwa huyo yupo mikononi mwa jeshi la polisi wilaya ya Makete kwa hatua zaidi za kisheria
Habari na Godfrey Martin, picha na Henrick Idawa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!