Thursday, 21 April 2016

Msongamano mahabusu wamtisha Dk. Mwakyembe


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema kuwapo kwa mahabusu wengi gerezani kunamtisha na kuonekana uendeshaji wa kesi kwenda kwa kusuasua.



Akizungumza mwishoni mwa wiki mkoani Geita, alikiri kuwapo kwa msongamano wa mahabusu na wafungwa gerezani kutokana na uchelewashaji wa upelelezi wa kesi za jinai na makosa mengine.
Akizungumza na wanasheria, mahakimu wa mahakama za Mwanzo wilaya na mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Geita, alisema hali ya uchelewashaji wa upelelezi wa makosa hasa ya jinai na madogo madogo kutokamilika kwa wakati na kusababisha msongamano mkubwa gerezani.
Alimuagiza mpelelezi wa makosa ya jinai nchini kufuatilia na kukamilisha upelelezi wa makosa mbalimbali kwa wakati na kutenda haki ili kuondoa msongamano huo.
“Hakikisheni wote mnaosimamia sheria na haki, mnapeleleza makosa kwa wakati mwingine serikali inaingia katika gharama zisizo za lazima kwa kuweka mahabusu wanaokabiliwa na makosa madogo ambayo ushahidi wake upo wazi,” alisema.
Awali, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Manzie Mangochie, alisema mkoa huo una mahakama za mwanzo 23, lakini 16 hazifanyi kazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za ukosefu wa majengo, vifaa na nyumba za watumishi kuwa chakavu.
Mangochie alisema gereza la wilaya ya Geita lina hadhi ya wilaya likiwa na uwezo wa kuhifadhi watu 197 kati yao 56 ni wanawake na wanaume 141, lakini kwa sasa lina mahabusu zaidi ya 500.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!