Sunday, 24 April 2016

Mnada wa Tanzanite wazalisha bilioni 1.3/-


SERIKALI imepata zaidi ya shilingi bilioni 1.3 katika mnada wa madini aina ya Tanzanite yaliyokamatwa na kutaifishwa serikalini, katika maonyesho ya tano ya Kimataifa ya madini ya vito na usonara.



Mnada huo ulifanyika juzi katika maonyesho hayo yaliyokuwa yakifanyika jijini hapa,na kutangazwa na Mkurugenzi wa uthaminishaji wa almasi na vito kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo.
Alisema kuwa mapato hayo yote hayo yaliyotokana na mnada huo yanaenda serikalini ambapo mnada huo uliongozwa na Kaimu Kamihsna wa Madini kutoka Wizara hiyo,Mhandisi Alky Samaje.
"Mapato yote hayo zaidi ya shilingi bilioni 1.3 yanaingia serikalini kwani madini hayo yalikamatwa na kutaifishwa na yalikuwa chini ya serikali tangu mwaka jana yalipokamatwa,"alisema
Mnada mwingine uliofanyika katika maonyesho hayo ulikuwa ni wa madini ya Tanzanite kutoka mgodi wa Tanzanite One na Stamico,madini ambayo yalikuwa hayajakatwa ambayo yaliuzwa na zaidi ya Dola Milioni 2.2 ambazo ni sawa na Sh bilioni tano za Kitanzania zimepatikana.
Kalugendo alisema kuwa katika mauzo hayo ya madini ya Tanzanite one,serikali inapata mrabaha wa zaidi ya Sh milioni 245.
"Katika fedha hizo zilizopatikana kutokana na mauzo ya Tanzanite kutoka mgodi wa Tanzanite One,serikali itapata mrabaha wa zaidi ya milioni 245 na matokeo ya mauzo ya maonyesho yote yatatangazwa na kamati ya maandalizi ila haya ni matokeo ya madini yaliyouzwa kwenye mnada tu,"alisema Kalugendo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!