Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, imepokea msaada wa madawaati 50 yenye thamani ya Sh. Tano kutoka kwa mke wa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Jackline Mengi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Hai, Renalda Ibrahimu, alipokea madawati hayo juzi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya halmashauri hiyo.
Akikabidhi madawati hayo, Mengi ameitaka jamii ishirikiane na serikali katika kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule zote nchini ili watoto wasiendelee kuteseka kwa kukaa chini.
Kwa upande, Renalda alimshukuru Mengi kwa msaada huo ambao utasaidia kupunguza tatizo la madawati katika wilaya hiyo, ambayo inakabiliwa na upungufu wa madawati 1,000
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Fred Kweka, alisema wilaya bado inakabiliwa na changamoto kutokana na baadhi ya wanafunzi kukaa chini, kutokana na upungufu huo.
Nipashe.
No comments:
Post a Comment