MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kitengo cha Ardhi, imetupilia mbali maombi ya kutaka kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi na kupinga bomoabomoa kwa wakazi 2,619 wa Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mahakama hiyo imeagiza Serikali kutoa elimu kwa wananchi hao ndani ya miezi minne kabla ya kuanza Oparesheni ya bomoabomoa, baada ya maombi ya wananchi hao kutupwa na mahakama.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Fredrica Mgaya.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Fredrica Mgaya.
Jaji Mgaya alisema mahakama yake imetupilia mbali maombi hayo kutokana na ombi la kwanza la kufungua kesi ya uwakilishi kutokuwa na mashiko ya kisheria.
Diwani wa Kata ya Tabata wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Patrick Asenga na wenzake tisa walifungua maombi hayo dhidi ya Manispaa ya Ilala, Baraza la Taifa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika maombi hayo namba 53 ya mwaka 2016, walalamikaji waliomba mahakama hiyo kutoa kibali cha kufungua kesi kwa niaba ya wenzao 2,619 wa kata za Tabata, Segerea, Liwiti, Vingunguti, Kipawa na Mnyamani kupinga operesheni ya bomoabomoa katika maeneo yao.
Pia, waliiomba mahakama hiyo itoe amri ya zuio la muda dhidi ya walalamikiwa kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali pamoja na kesi ya msingi watakayoifungua.
“Katika ombi la kwanza, lilikuwa halina mashiko ya kisheria, walalamikaji hawakuwasilisha orodha ya majina yaliyokuwa na sahihi ili kuonyesha wameridhia kufunguliwa kwa kesi ya uwakilishi," alisema Jaji Mgaya.
"Hiyo ni hitilafu kisheria kwa kuwa walalamikaji hao hawajaonyesha kama kuna ridhaa na wamekubaliana na wawakilishi wao kama wanahitaji kufungua kesi. Mahakama imeona maombi hayo hayana mashiko ya kisheria na inayatupilia mbali.
"Kwa upande wa maombi ya zuio la muda la kutobomolewa, kimsingi halitakuwa na nguvu kutokana sababu nilizoeleza awali.”
Jaji huyo aliiagiza serikali kupitia NEMC kuwapa elimu kwa muda wa miezi minne wananchi hao ili waweze kujipanga kabla ya kuanza mchakato wa kuwabomolea nyumba zao.
Alisema kwa kawaida mahamakama haiwezi kuiwekea pingamizi Serikali kutotekeleza majukumu yake, isipokuwa katika hali ya ubinaadamu inaweza kuingilia kati.
“Kinachotakiwa kufanyika sasa ni ubinadamu tu, ndani ya miezi minne ninayowaomba inatakiwa muwape elimu wananchi kuhusu athari za maeneo hayo sambamba na kuwapa maelezo waende wape,” alisema Jaji Mgaya.
Jaji Mgaya alibainisha kuwa haitakuwa vyema kwa Serikali na walalamikaji hao wakaendelea kuzozana mahakamani, hivyo inatakiwa ifikie hatua wakae chini na kuzungumza juu ya mustakabari wa kusaidiana.
Hata hivyo, Jaji Mgaya alisema wananchi hao bado wanayo nafasi ya kujipanga na kufanya marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili kufungua kesi nyingine.
“Mnaweza kufungua kesi endapo mkifanya marekebisho isipokuwa siwashauri mfanye hivyo," alisema Jaji Mgaya. "Badala yake mkae mzungumze.
"Kama kuna watu wamepewa viwanja, naomba waende maeneo waliyopewa, badala ya kuja mahakamani kutaka mlipwe fidia mara mbili.”
MAJONZI VIUNGANI
Katika viunga vya mahakama hiyo; baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, waanchi hao walionekana kukaa katika makundi tofauti huku wakionekana wenye majonzi na kuwahoji maswali mbalimbali mawakili wao.
Katika viunga vya mahakama hiyo; baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, waanchi hao walionekana kukaa katika makundi tofauti huku wakionekana wenye majonzi na kuwahoji maswali mbalimbali mawakili wao.
Mawakili walitumia muda kuwaelewesha na kuwatuliza kwamba inawezekana wakajipanga kufungua upya maombi mengine.
No comments:
Post a Comment