Pages

Friday 8 April 2016

Mahakama ya Kisutu leo yakataa kuwaachia kwa dhamana, Kamishna Mstaafu wa TRA Harry Kitilya na wenzake Shose Sinare na Sioi Sumari


Mahakama ya Kisutu leo yakataa kuwaachia kwa dhamana, Kamishna Mstaafu wa TRA Harry Kitilya na wenzake Shose Sinare na Sioi Sumari, makosa yao hayana dhamana.
-Walishtakiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka na utakatishaji fedha



Korti ya Kisutu leo yakataa kuwachia Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba na Waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare kwa kuwa mashtaka yao hayana dhamana.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), tarehe 1/4/2016 iliwafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote walishtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

No comments:

Post a Comment