Friday 22 April 2016

Mabasi yaendayo haraka yaanza kazi Rasmi


Mabasi 50 yanaanza kazi rasmi Ijumaa April 22,2016.Ratiba ndefu imetangazwa. Lakini Lakini Kiwango Cha Nauli Hakijawekwa Wazi. Kulikoni? Zisije Kuletwa Zile Za Awali Maana Rais Alishazikataa Juzi Wakati Anazindua Fly Over Pale Tazara.
Ratiba Hii Hapa Chini:




MABASI YATAANZA SAFARI SAA KUMI NA MBILI KASORO ROBO ASUBUHI IJUMAA APRIL 22,2016, KUTOKEA DEPOT YA JANGWANI KWA MPANGILIO UFUATAO.

1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.

2. RUTI YA KIMARA - KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO - KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.

5. RUTI YA UBUNGO - MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

6. RUTI YA MOROCCO - KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)

3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

JUMLA NI MABASI HAMSINI (50)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!