Pages

Friday, 1 April 2016

KAMISHNA MKUU WA MAPATO MSTAAFU NA WENZAKE WATUPWA RUMANDE KWA UBADHILIFU WA BILIONI 12

Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya (wa pili kushoto) na wenzake Shose Sinare na Sioi Solomoni wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaamu leo wakikabiliwa na mashitaka 8 ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 6, kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda serikalini. Watuhumiwa hao wamepelekwa rumande mpaka Aprili 8 itakapotajwa tena.








Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Harry Kitilya na wenzake Shose Sinare na Sioi Solomoni wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaamu leo wakikabiliwa na mashitaka 8 ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda serikalini.


Watuhumiwa hao wamekana makosa na kurudishwa rumande hadi April 8, 2016 kesi yao itakapo somwa tena na Mahakam kuweka wazi juu ya suala la dhamana.

No comments:

Post a Comment