Monday, 4 April 2016
ISMAIL MUSA SUMAJR NA MASHAIRI YA MAPENZI
DEMU WANGU WA KWANZA:
Hatungonoka ni love bila matusi, alisema mapenzi ya kweli hayahitaji kupiga mikasi
Kumuona na kumbusu kwangu ilikuwa tosha sana, nikakubali sina haraka nisimpoteze kimwana
Nilimtaka utotoni nikajampata ukubwani, labda ndio maana haikuniuma alishanitoka moyoni
Mi nilimega kinguonguo pumbavu wakafanya kweli, wa kwanza kuniliza wa kwanza kunikubali
Mungu angependa pengine ndiye ningemuoa, sikumbuki hata aliniacha vipi ghafla ashapotea
Wote wanaokuja sema hawaelezi yu pande gani, Nasikia kashazalishwa ila sifahamu na bwege gani
Sisemi namchukia ila kweli simpendi tena, hata nikitaka kuoa sio yeye ashakuwa mama, wakati tu naukumbuka japo nafahamu haurudi, Historia nishaiandika naikubali sina budi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment