Tuesday 5 April 2016

IKIWA NI ZIARA YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI,RAIS MAGUFULI KUSAFIRI KWA GARI BADALA YA NDEGE KUELEKEA RWANDA

Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. RaisMagufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagamewa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.


Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na RaisKagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzaniana Rwanda na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania RaisMagufuli atasafiri kwa gari.
2
Kutoka kushoto ni Rais Magufuli na Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbali ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais Kagame mjini Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.
KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!