Monday, 11 April 2016

Bunge limebana matumizi limeokoa hizi bilioni ambazo zimerudishwa kwa watanzania....

April 11 2016 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, John  Pombe Magufuliamepokea taarifa ya taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa ‘Takukuru’ na hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.


Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo, ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati. 
Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.
1
Rais Maguli akipokea taarifa ya mwaka ya Takukuru kutoka kwa Mkurugenzi Kamishna Valentino Mlowola
2
Rais Magufuli na Naibu Spika Tulia Ackson
4
.
3
.
5
.
6
.
8
.
7.
.
9
10
11 12
Kwa hisani ya Millard Ayo.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!