Tuesday, 12 April 2016

Baada ya kukwepa kodi kwa miaka mitatu mfululizo, kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Acacia imesema inatarajia kulipa kodi ya zaidi ya Sh40 bilioni mwaka huu wa fedha.



Baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi kwa miaka mitatu mfululizo, kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Acacia imesema inatarajia kulipa kodi ya zaidi ya Sh40 bilioni mwaka huu wa fedha.




Mwishoni mwa Machi, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) iliitaka African Gold Mine (kwa sasa Acacia) kuilipa Serikali kodi ya Dola za Marekani 41.25 milioni (zaidi ya Sh89 bilioni), lakini kampuni hiyo ilikata rufaa na shauri hilo linasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Acacia inayomiliki Kampuni tatu ndogo za Bulyanhulu Gold Mining, North Mara na Pangea Minerals zinazoendesha shughuli zote za mapato ya mchimbaji huyo mkubwa kuliko wote nchini ambaye anaelezwa kukwepa kodi ya zuio la malipo ya gawio kwa wanahisa wake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon ambaye aliwasili jana ili kutembelea miradi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wake, alisema Acacia bado haijaanza kutengeneza faida za kulipa kodi ya Mapato ya Kampuni kwa kuwa bado haijarudisha mtaji wake wa awali.

“Pamoja na kwamba tunatengeneza faida kwa jumla, hiyo haitozwi kodi kwa sababu bado hatujarudisha mtaji wa Dola za Marekani 3.8 bilioni. Mkataba wetu na Serikali ya Tanzania unaonyesha kuwa tutatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia mwaka 2018,” inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na Gordon.

Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika alisema kuwa kampuni hiyo inaanza kulipa kodi ya mapato mwaka huu baada ya kurejesha mtaji wake iliyowekeza kupitia kampuni yake ya North Mara. “Tumerudisha mtaji wetu na makadirio yanaonyesha tunaweza kulipa kodi ya Dola 20 milioni za Marekani (zaidi ya Sh40 bilioni). Nusu ya kiasi hicho tayari kimeshapelekwa TRA,” alisema.


Chanzo: Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!