Sunday 27 March 2016

WAZIRI ATOA SIKU 7 KWA MAKAZI YA VIGOGO


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, ametoa siku saba kwa watu wanaotiririsha maji taka kwenye mitaro ya kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kuacha mara moja, kinyume chake hatua kali zitachukuliwa.

Sehemu kubwa ya kitongoji cha Mikocheni ni la viwanja vya makazi ya watu wachache, na wengi waliojenga ama kuishi huko ni wenye hadhi serikalini au kwenye jamii.
Mpina aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya usafi katika mtaa wa TPDCb kata ya Mikocheni, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Alisema ameshangazwa kuona watu wakitiririsha maji katika mitaro hiyo ambayo imekuwa na harufu mbaya, hali ambayo inachafua mazingira na kufanya wananchi wa eneo hilo kuishi katika mazingira magumu.
Alisema mabomba ya Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka (Dawasco) yamepasuka na kutiririsha maji machafu ambayo yana kinyesi.
Aidha, watu wenye viwanda hupitisha maji katika mitaro hiyo, aligundua Waziri Mpina, ambaye alisema ilitakiwa kupitisha maji kama mvua zinanyesha.
Badla yake, kila siku maji machafu yanatiririka kwenye mitaro hiyo hivyo kuweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Mpina amemuagiza Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha ndani ya siku saba anashirikiana na Dawasco kusimamisha maji hayo kupita katika mtaro huo.
Aidha, Mpina alisema viwanda ambavyo vinatiririsha maji hovyo na kuchafua mazingira vitafungiwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema hivi karibuni ataanzisha oparesheni maalumu ya siku 30 ili kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa katika hali ya usafi kwa sababu mwamko bado ni mdogo.
“Nimeshangaa nilimualika Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya awepo katika eneo hilo lakini hawajafika na taarifa hawajanipatia," alisema Mpina. "Hata hawa wa Dawasco walitakiwa kuwepo waone hili suala.”
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mhandisi Bonventure Baya alisema wataanza kulishughulikia suala hilo kwa kukaa meza moja na Dawasco ili kusitisha maji hayo yasiendelee kutiririka katika mtaro huo.  
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu alisema wahusika hao ambao ni wachafuzi wa mazingira sheria ipo wazi kwani wanatakiwa kuchukuliwa hatua ama 
NIPASHE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!