Friday, 18 March 2016

Watu 9 walazwa zahanati ya Mpekenyela kwa kula samaki wenye vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu.



Watu tisa wamelazwa katika zahanati ya Mpekenyela wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi baada ya kula samaki wanaosadikiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu na kuwasababishia kuhara na kutapika na  kupoteza nguvu.


Kufuatia tukio hilo wafanyabiashara wawili wa Samaki katika kata ya Mpekenyela na Namungo wilaya ya Ruangwa Somoe Kishoka na Fatuma Saidi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuuza samaki wenye vimelea vya Kipindupindu.
 
Akizungumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa zahanati ya Mpekenyela Mikidad Mbule  anathibitisha kupokea wagonjwa hao,huku ndugu wa mgonjwa aliyelazwa  kutokana  na maambukizi anaelezea hali hiyo ilivyomkuta. 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!