Wednesday 23 March 2016

UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA



Anemia na madini chuma

Uchovu, udhaifu, na kupumua haraka haraka kawaida husababishwa na anemia — ukosefu wa madini chuma katika damu.


Anemia hujitokeza zaidi miongoni mwa wanawake, ambao hupoteza madini chuma kupitia damu ya hedhi. Anemia inaweza kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa wadogo sana na hatari zaidi kutokana na damu nyingi ambayo hupotea wakati wa kujifungua. Kipimo cha damu kwa ajili himoglobini hupima kiwango cha madini chuma katika damu.

Dalili za anemia

  • Rangi ya fizi na sehemu ya ndani ya kigubiko kupauka au kufifia
  • Kukosa nguvu
  • Uchovu
  • Kizunguzungu
  • Matatizo katika kupumua



Matibabu na kinga



Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi:
  • Maharagwe, njegere au kunde, na dengu
  • Mboga za kijani na mwani
  • Matunda yaliyokaushwa
  • Mbegu na njugu
  • Aina yote ya nyama ikiwemo nyama ya kuku au bata, samaki, samakigamba(shellfish), au wanyama wadogo.

Nyama za viungo vya ndani kama vile maini na moyo, na vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganywa na damu kawaida huwa na kiwango kikubwa cha madini chuma.
Mtu yeyote ambaye rangi yake ya ngozi inaonekana kupauka au kufifia, mchovu au dhaifu, au ambaye ametokwa sana na damu anaweza kuwa na anemia kali. Anahitaji kumuona daktari na ikibidi kupatiwa vidonge vya madini chuma (iron pills).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!