Monday 28 March 2016

Serikali yaandaa muongozo wa ajira kwa vijana



Mkurugenzi msaidizi Taasisi ya soko la ajira Ofisi ya Waziri mkuu kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Ahmed Makbel

 
Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel wakati akizungumza na East Africa Radio kuhusu mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza kuchukuliwa ili kuhakikisha inawainua vijana kiuchumi.
Makble amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana na Serikali ili waweze kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha na kipato kizuri pamoja na mazingira mazuri ya kazi.
Mkurugenzi huyo amesema serikali imeanza kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia kwenye vipato vyao vya kila siku sambamba na kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.
Makbel ameongeza kuwa wahusika wakuu wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe mazingira rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa yakuchangia pato la taifa na serikali kuu wameanza vikao vya pamoja ili waone wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa vijana.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!