Wednesday, 2 March 2016

Rais Magufuli aomboleza kifo cha kaka wa Kikwete.


Rais John Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi, Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, kwa kifo cha kaka yake, Mzee Selemani Kikwete, kilichotokea nchini India wakati akipatiwa matibabu.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa jana, Rais Magufuli amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na kwamba anaungana na familia ya Kikwete katika maombolezo ya msiba huo.
 
“Napenda kukupa pole Rais Mstaafu, Kikwete, familia yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika familia, natambua uchungu mlionao, lakini nawaomba muwe na uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu ,” alisema Rais Magufuli.
 
Rais Magufuli pia amemuombea Marehemu Mzee Kikwete apumzike mahali pema peponi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!