Tuesday 29 March 2016

Mshukiwa wa bomu la Brussels aachiwa huru

Image copyrightBelgian Federal Police
Image captionMshukiwa mkuu wa bomu la Brussels aachiwa huru
Afisi ya kiongozi wa mashtaka nchini Ubelgiji imemuachilia huru mshukiwa mkuu wa mashambulio ya bomu yaliyotokea juma lililopita jijini Brussels.


Kingozi wa mashtaka ya umma anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa mtu anayetambuliwa kama Faycal C ndiye mshukiwa mkuu aliyenaswa na kamera fiche (CCTV) katika eneo lililoathirika.
Afisi hiyo inasema hadi kufikia sasa hizo zilikuwa ni madai tu dhidi ya bwana huyo.
Faycal C alikamatwa baada ya mtu kuielezea polisi kuwa alimshuku kuwa ndiye aliyeonekana katika picha fiche CCTV katika uwanja wa ndege wa Zaventem muda mchache kabla ya mlipuko huo uliosababisha maafa makubwa.
Kufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji wa kujitolea mhanga akiwa amevalia kofia.
Image copyright
Image captionKufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji
Kauli hiyo ya afisi ya kiongozi wa mashtaka imetupilia mbali matumaini ya kumkamata mshukiwa halisi aliyekwepa kutoka eneo la tukio baada ya shambulizi lililoua zaidi ya watu 35.
Ibaada ya makumbusho imeratibiwa kufanyika usiku kutwa katika kanisa kuu mjini Brussels.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!