Thursday, 31 March 2016

MILLEN MAGESA AFANYA SEMINA YA UGONJWA WA ENDOMETRIOSIS

Millen Magese akiwa na Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala

Mwanamitindo wa kimataifa ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2001, Millen Happiness Magese Jumatano hii amefanya semina maalum kwa vijana wa sekondani wapatao mia tano pamoja na walezi wao 100 kuhusu ugonjwa wa Endometriosis.


Katika semina hiyo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala.
Akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika katika shule ya sekondari Turiani Magomeni Dar es salaam, Millen ambaye pia ni mhanga wa ugonjwa wa Endometriosis, amesema ameamua kufanya semima hiyo kwa vijana ili kuwapa uwezo wa kutambua dalili za ugonjwa huo mapema kabla hauja waathiri zaidi na kuwafanya kuwa wagumba kama yeye.
“Leo nimeamua kufikisha ujumbe huu kwa taifa langu kwa kutumia taasisi yangu ‘Millen Magese Foundation’ ili kuelisha jamii juu ya ugonjwa wa Endometriosis. Lengo kuu sio tu kuwafikia nyie mliopo hapa, kwa sababu hapa kuna wanafunzi mia tano, walezi na wazazi 100 lakini kupitia umati huu nitawafikia watu zaidi ya elfu kumi, kwa maana ya kila mmoja atafikisha ujumbe kwa watu zaidi ya ishirini,” alisema Millen.
Pia mrembo huyo ambaye harakati zake za kupambana na ugonjwa wa Endometriosis zimempa tuzo ya BET, Music Meets Runway Global Award (MMR) pamoja na kutajwa kama BBC Unsung Hero 2015, alisema ana mpango wa kujenga hospitali nchini kupitia taasisi yake itayokuwa inashughulikia ugonjwa Endometriosis.

Kwa upande wa mgeni rasmi, Dkt. Khamis Kigwangala alimpongeza Millen Magese pamoja na kutoa ahadi ya kushirikiana naye ili kutimiza malengo yake.



Afisa elimu Sekondani wa Manispaa, Rogers .J. Shemwelekw




Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akiwa na mwanamitindo, Ally Daxx



Wanafunzi


Daktari kutoka Muhimbili akielezea dalili na chanzo cha ugonjwa wa endometriosis














No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!