Tuesday, 15 March 2016

MBARONI KWA KUJIANYA MAOFISA WA TRA


Watu waatatu, akiwamo askari polisi wa kituo cha Mbagala Kijichi, jijini Dar es Salaam, wamekamatwa kwa kujifanya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
 
Watuhumiwa hao walikamatwa Machi 10, mwaka huu wakiwa katika   maduka ya kijiji cha Kigululu, wilayani Mkuranga wakiwatoza kodi na kujifanya kukagua vitabu vya mauzo.
 
Ofisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa TRA Mkoa wa Pwani, Bakar Kapera, alisema kabla ya kukamatwa watuhumiwa hao walipita kijiji cha jirani na kujitambulisha wametokea Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanznaia (TFDA), awali wakidai wametokea TRA.
 
Wakiwa katika kijiji cha Kigululu, Kapera alisema walianza kuwadai wamiliki wa maduka taarifa za mauzo huku wakitaka walipe kodi,. Ndipo wananchi hao walipowashtukia na kupiga simu polisi hatimaye kukamatwa.
 
Aliwataja watuhumiwa hao ni pamoja na derava wa gari walilokuwa wakitumia aina ya Toyota Noah,  lenye namba za usajili T 378 DCR, Hausi Issa au hamisi Zuberi (jina lilolomo katika kitambulisho cha kupigia kura),  alitambulika kwa jina la Hamis Zuberi(29), mkazi wa Mbagala Kibulugwa.
 
Mtuhumiwa mwingine ni Ramadhani Ndimbo (53) ambaye katika kitambulisho feki  cha TRA alikuwa na jina la Issa Kipangapori mkazi wa Kimara. Askari polisi aliyekamatwa alifahamika kwa jina la Godwin.
 
Kapera alisema kabla ya kukamatwa, walipita katika  vijiji vya Chabuku na Mamlikongo, wakiambatana na askari ili kufanikisha mpango wao huo wa kujipatia fedha kwa kujifanya wafanyakazi wa TRA.
 
Aidha, Kapera alisema watuhumiwa hao awali walikua sita lakini watatu kati yao walikimbia katika purukushani na polisi.
 
Alisema wakati wakifanya kazi hiyo, walikuwa wakitumia vitambulisho vya TRA na TFDA. Alisema walikuwa wakitumia fomu za TFDA, fomu za uthibitisho wa mlipakodi (VRN) na fomu za usajili wa mlipakodi (TIN) katika kukusanya kodi kama maofisa wa TRA.
 
Inaelezwa kuwa kabla ya kukamatwa, watuhumiwa hao walifanikiwa kuchukua vipodozi dazani tano kwenye duka la vipodozi la Amina huko Mkuranga, wakidai vimeisha muda wa matumizi.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventura Mushongi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watachukuliwa hatua za kisheria baada ya kukamilika upelelezi. 
 
Mushongi alisema askari aliyekamatwa akihusishwa na tukio hilo, hakutumwa kufanya kazi hiyo, hivyo hatua za kinidhamu zitafuata baada ya taratibu kukamilika.
 


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!