Jide ambaye amepotea kwenye tasnia kwa takriban mwaka mmoja, anatarajiwa kuachia albamu hiyo Jumamosi hii ikiwa imebeba jina la ‘Naamka Tena’.
Meneja wa msanii huyo, Christine Mosha alisema maandalizi yote yamekamilia, kinachosubiriwa ni siku husika.“Hii ni albamu ya saba tangu aanze muziki, mashabiki wake wajiandae kupata mambo mazuri zaidi baada ya kukaa kimya muda mrefu kwa sababu komando anarudi na nguvu mpya kama jina la albamu linavyojieleza,” alisema Mosha.
Kwa muda mrefu nyota huyo amekuwa kimya kwenye muziki na kujikita zaidi kwa masuala ya familia, hivi karibuni mahakama ilivunja rasmi ndoa yake na Mtangazaji wa redio, Gadner Habash.
Albamu zake zilizotangulia ni Machozi, Binti, Moto, Shukrani, Ya tano na Nothing But the Truth
No comments:
Post a Comment