Thursday, 31 March 2016

JINSI YA KUMSAIDIA MTU ALIYEKABWA NA KITU




Mtu alieyekabwa ambaye hawezi kukohoa au hawezi kuongea pia hawezi kupumua. Unaweza kuponya maisha yake kwa kumsaidia haraka. 

Mpige makofi mgongoni
Mwinamishe kwa kumpinda eneo la nyonga, na kumpiga makofi ya kushindilia 5 katikati mgongoni, kati ya mifupajembe (shoulder blades) ya mabegani. Tumia kiganja cha mikono yako.

Kama hili halitasaidia:
Mmbinye tumboni
Simama nyuma ya majeruhi na kuzungusha mikono yako kiuno chake.

Weka mkono wako ukiwa umekunjwa kama ngumi dhidi ya tumbo lake, juu kidogo na kitovu na chini ya mabavu.

Funika ngumi yako na mkono ule mwingine na kuitumia mikono yote 2 kubinya kwa nguvu na haraka juu na ndani. Tumia nguvu ya kutosha kumwinua majeruhi juu ya miguu yake. (Tumia nguvu kidogo kiasi kwa ajili ya mtoto mdogo.) Rudia zoezi mara 5 mfululizo.

Kama kuna kitu ambacho kinazuia hewa kufika kwenye mapafu au kooni, nguvu ya hewa ambayo inasukumwa kwa mkazo inapaswa kukiondoa.
Kwa mwanamke mjamzito au mtu yoyote mnene, weka mikono kuzunguka sehemu ya kati ya kifua chake (weka ngumi yako katikati ya maziwa). Halafu binya kwa ndani.

Kama majeruhi atapoteza fahamu

Taratibu mlaze chini kwenye mgongo wake na angalia ndani ya mdomo wake. Kama utaona chakula au chochote kinachoziba koo, kiondoe kwa kutumia kidole ambacho umekunja kama ndoana. Lakini usisukume ndani kwa sababu hii inaweza kusababisha kitu kinachoziba kooni kuingia ndani zaidi. Halafu sukuma kwa nguvu na haraka eneo la kati kifuani hadi atakapoanza kupumua.

Kwa mtoto zaidi ya mwaka 1

Kama mtoto anakabwa na hawezi kulia wala kukohoa, jaribu kuzibua koo lake kwa kumpa makofi mepesi yenye mkazo mgongoni na mibinyo ya kifuani.
Mweke mtoto inavyopasa
Mkamate mtoto ukiangaliza uso wake chini na sehemu ya kichwa ikiwa chini kidogo kuliko mwili wake mwingine.

Mpe makofi mepesi yenye mkazo mgongoni 
Tumia shina la kiganja chako kumpa makofi 5 mepesi lakini yenye mkazo kati ya mifupajembe mabegani.

Kama mtoto hataanza kupumua, mgeuze angalie juu.


Mmbinye kifuani
Weka vidole 2 au 3 katikati kifuani — chini kidogo ya chuchu.


Binya kifuani kwa mkazo kiasi harakaharaka angalau kufikia sentimeta 2. Binya angalau mara 5 au hadi mtoto atakapoanza kupumua.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!