Friday 18 March 2016

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEZAMA MAJI



Kuzama majini

Mtoe mtu kwenye maji haraka iwezekanayo na bila kuchelewa anzisha pumzi maalum ya uokozi namibinyo kifuani. Toa pumzi za uokozi kwanza ili kuingiza hewa kwenye mwili wa mgonjwa.

Kama mgonjwa atatapika, mgeuze alaliye upande na pole pole tumia kidole chako au kitambaa kupangusa matapisi ili asije kukabwa.

Pumzi maalum ya kuokoa maisha

Watu wanaweza kuishi kwa dakika 4 tu bila kupumua. Unaweza kunusuru maisha ya mtu mwingine kwa pumzi maalum za kuokoa maisha kama pumzi yake itasimama kwa sababu ya kukabwa, kupigwa kichwani, kukaribia kuzama, au kupigwa na shoti ya umeme, kuzidiwa na dozi ya dawa au akiwa na baridi kali (hypothermia).
Kama mtu atashindwa kupumua, unaweza kuponya maisha yake kwa kumpatia pumzi maalum ya kumuokoa mara moja.



Weka kichwa chake katika nafasi inayotakiwa
Mlaze uso wake ukiwa unaangalia juu. Inua kidevu chake na kusukumzia eneo la paji la uso kuinua na kulaza kichwa ili pua yake iwe inaangalia juu.





Mpe pumzi za kuokoa maisha
Bonyeza na kufunga pua yake ili hewa isitoroke kupitia njiahiyo.
Funika kabisa mdomo wake kwa kutumia mdomo wako.
Mpe pumzi 2 za nguvu, zikienda polepole.
Kifua kinapaswa kuinuka kila anapopokea pumzi. Kama hakitainuka, hewa itakuwa haingii kwenye mapafu. Badilisha kidogo jinsi kichwa kilivyokaa na kujaribu tena. Wezesha mgonjwa kupumua nje mwenyewe kila unapompa pumzi ya uokozi.



Chunguza mapigo ya moyo
Baada ya pumzi 2, chunguza iwapo anapumua. Jaribu kuchunguza mapigo ya moyo kila upande wa shingo, au sikilizia kifuani, au juu ya moyo.

Kama hakuna mapigo ya moyo, angalia "Pasipo Mapigo ya Moyo"
Kama unahisi kuwepo mapigo ya moyo au mapigo ya moyo kusikika bayana, endelea kumpa pumzi za uokoaji hadi atakapopumua mwenyewe. Hii inaweza kuchukua dakika 30 au zaidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!