Homa ya manjano ni ugonjwa unawashika watoto wachanga baada ya masaa machache kuzaliwa .Manjano kawaida huonyesha rangi ya manjano kwenye macho ,paji la uso,nyayo za miguu,kifuani na tumboni ,ukimkagua mtoto vizuri haswa kwenye mwaga wa jua utaona wanjano kwa urahisi.Homa ya manjano inashika watoto na watu wazima pia.
Mtoto ataonyesha dalili tofauti ,anaweza akaonyesha zote kwa pamoja au baadhi yake,
: Macho ya mtoto na ngozi kubadili rangi kuwa ya njano
:Homa kali
:Kutapika
:Kulala sana
:Mkojo kuwa brown
Ukiona hizo dalili ni hatari muwaishe hospital.
Hali ya mtoto kuwa wanjano kitaalamu inaitwa Jaundice,husababishwa na kemikali inayoitwa bilirubin kuzalishwa kwa wingi kwenye damu ya mtoto.Bilirubin inapokuwa nyingi kumletea mtoto madhara . Takwimu inaonyesha watoto wakiume ni rahisi kupata manjano kuliko watoto wa kike,na asilimia 80 ya watoto njiti hupata homa ya manjano wakiwa na siku 5 mpaka 7 baada ya kuzaliwa .
Sababu zinazomfanya mtoto apate manjano Jaundice
1: Mtoto anapokuwa na blood group tofauti na mama ,anakuwa na hatari ya kupata manjano.
2:Mtoto njiti premature ni rahisi kupata manjano
3:Watoto waliozaliwa na matatizo ya kiafya au infection
4:Mama wenye blood group o wanahatari ya kusababisha mtoto kupata manjano
5: Mama anaepata kisukari kipindi cha mimba )gestational diabetes anaweza zaa mtoto mwenye manjano.
6:Mama kuzalisha maziwa machache kunaweza msababishia mtoto kupata manjano
7:Mtoto mwenye matatizo ya ini nao hupata manjano
Matatizo ya kiafya anayopata mtoto aliepata manjano
Mtoto anapopata manjano ni vizuri kutibiwa haraka iwezekanavyo ,lasivyo mtoto atapata haya matatizo
:Kemikali ya bilirubin ikiongezeka sana kwenye damu ya mtoto inaenda adhiri ubongo
: kumsababishia matatizo ya kuto kusikia,
:kuto kuona
:Kushindwa ongea na kutembea vizuri
:Kifo
:Ulemavu wa kudumu
TIBA
Manjano hutibika kwa njia tofauti , na huchukua siku 7 mtoto kupona iwapo hatokuwa nayo nyingi mwilini,kama ni nyingi itamchukua zaidi ya siku saba.
1:Maziwa ya mama ni tiba kubwa, mama anatakiwa kunyonyesha mtoto kwa wingi ili kupunguza kiasi cha billirubin iliozalishwa kwa wingi kwenye damu ya mtoto. Mtoto atolewe nje apigwe na jua , jua linasaidia kupunguza ile sumu.
2: Mtoto,atawekwa kwenye kifaa kiitwacho Phototheraphy light kwa masaa 48 au zaidi mpaka daktari atakapo ona sumu imeisha mwilini.
anapokuwa kwenye phototheraphy anafunikwa macho ili ule mwanga usimwadhiri macho yake na kuveshwa diaper tu ili mwanga na hilo joto kuzuia mzunguko wa billrubin kwenye damu ya mtoto.
3: Njia nyingine ni kubadilishwa damu ila hii atafanyiwa iwapo hali yake inaonyesha ni mbaya zaidi.
NB
Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto hakikisha unamnyonyesha kila baada ya masaa 2 ili kuondoa manjano kwa haraka na kusave maisha ya mtoto,kama maziwa hayatoki hakikisha unamnunulia baby formula )maziwa ya kopo.
SHUKRANI KWA AFYA YA MTOTO.
No comments:
Post a Comment