Akiongea kwa uchungu kwenye kipindi cha Da Weekend Chat Show cha Clouds TV jana, Chidi ambaye mwili wake umepungua kwa kiasi kikubwa, amesema bado uwezo kimuziki anao lakini wale aliowaita wadau walioushikilia muziki wamemtupa.
Amesema wakati wa kilele chake, alikuwa akifanya show kila siku katika wiki, lakini kwa sasa mambo yamebadilika kabisa. “Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Chidi amedai kuwa kuna watu wanaamini kuwa kama akiwa juu, wasanii wengi wa hip hop watakuwa na wakati mgumu. “Hawa Joh Makini sijui, nani wanakuwa hawapo. Sasa hakuna mdau anayeweza kukubali akina Joh Makini wasikuwepo awepo Chidi Benz peke yake,” alisema.
Katika hatua nyingine Chidi alisema pamoja na afya yake kuzorota, hivi karibuni alipiga show kwa masaa mawili hadi mama yake akalia. "Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie' na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond," alisisitiza.
No comments:
Post a Comment