Watu wawili wamefariki dunia wakati wakivua samaki katika mto Ruvuma huko Mkenda mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambapo mwili wa mtu mmoja umepatikana huku wananchi wakiendelea kuutafuta mwili mwingine.
Watu waliofariki katika mtu Ruvuma wametajwa kuwa ni Said Mapanja ambaye mwili wake umeshapatikana na Bruno Ngaponda ambaye mwili wake bado unatafutwa na wote wana miaka thelasini na mbili ambapo ITV imezungumza na baba mzazi wa marehemu Bruno Bw. Edmund Ngaponda ambaye anaeleza jitihada zinazofanyika katika kusaka mwili wa mwanae katika mto Ruvuma hadi mto msinji unaokutana na mto Ruvuma.
Wananchi waishio mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika maeneo ya Nakawale na Mkenda wanasema kuna vifo vingi vinatokea katika mto huo ambapo ndani ya miaka mitano watu zaidi ya kumi wamekufa katika mto Ruvuma na hakuna viongozi wa serikali wanaowatembelea kuwapa pole hivyo wameipongeza ITV kwa kuwatembelea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma kamishna msaidizi wa Polisi ACP Zuberi Mwombeji amesema taarifa za watu kufa maji mto Ruvuma bado hajazipata na hivyo atafuatilia tukio hilo.
No comments:
Post a Comment