Monday, 22 February 2016

WATANZANIA WAPATA FURSA YA KUJIUNGA NA ELIMU YA JUU KWA VYUO VYA NJE.

ed1
Mshauri wa masuala ya Elimu kutoka Taasisi ya Aryan International Education Consultants ya nchini China Dkt. Safdar Khattak akitoa maelezo kuhusu namna ya kujiunga na Elimu ya Juu kwa wanafunzi wakitanzania waliotembela maonyesho ya Kimataifa ya Elimu “Tanzania Internation Education Fair 2016” yanayoendelea katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.


ed2
Mmoja wa wadau wa elimu aakijaza fomu ya kujiunga na Chuo Kikuu cha  BPP cha nchini Uingeraza alipotembelea maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 jana jijini Dar es Salaam.Wanaomshuhudia ni Afisa Mtendajji Mkuu wa Taasisi ya WR Education Placement Consultant ya nchini Bw. Robert (kulia) na Mshauri wa Wanafunzi wa Education Placement Consultant Bi. Berinda.
ed3
Mwakilishi wa Taasisi ya Sta Travel inayojihusisha na kusafirisha wanafunzi kwa punguzo ya gharama za usafiri Bw. Abbas Karrim akisikiliza maoni kutoka kwa baadhi ya wadau wa elimu waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
ed4
: Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Eastern Medeterrenian cha nchini Uturuki akiwapa maelekezo wanafunzi wakitanzania waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
ed5
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Thompson cha nchini Canada Bi. Brenda Nicole akiwapa maelekezo wanafunzi wakitanzania waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
ed6
Baadhi ya wanafunzi wakipitia machapisho ya vyuo mbalimbali  waliotembelea maonyesho yaTanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija
……………………………………………………………………………………………………………………
Na: Frank Shija, MAELEZO
Watanzania wanaosoma masomo ya elimu ya juu nje ya nchi kunufaika na gharama ndogo zenye punguzo maalum za kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi wanazo somea kupitia Taasisi ya Sta Travel ya jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Taasisi ya Sta Travel Abbass Karim wakati wa monyesho ya Tanzania International Education Fair 2016 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Abbas amesema kuwa taasisi yao imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo.
Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi nhasa wanafunzi wanaoenda kusoma Kuala Lumpar Malyasia, London Uingereza, na Guangzhou China.
Aidha Abbas alisema kuwa pamojja na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.
Kwa upande wake mtanzania aliyenufaika na kupitia Taasisi hiyo Bw. Ally Abdallah amesema kuwa binafsi anaipongeza taasisi hiyo kwa kuwa imemuwezesha kusafirikwa gharama nafuu ambazo kwake zilikuwa rahisi kuzimudu tofauti na gharama halisi ya usafiri kwa kawaida.
Sta Travel ni Taasisi inayojihusisha na utoajji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama nafuu yenye punguzo maalum kwa leongo la kuwasaidia watanzania kufikia ndoto zao bila kuwapo na kikwazo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!