Thursday 4 February 2016

WASIOAMINI MUNGU YUPO WADAI KUBAGULIWA KENYA


Kundi moja la watu wasioamini kwamba Mungu yupo linasema kuwa limebaguliwa baada ya serikali kukataa kulisajili.

Liliambiwa kwamba ombi lao lilitupiliwa mbali kutokana na wasiwasi kwamba hatua hiyo itavuruga amani na utulivu nchini.
Wanachama hao walio 60 nchini Kenya waliwasilisha ombi la kutaka kutambuliwa rasmi mwaka jana. Zaidi ya asilimia 97 ya Wakenya wanajitambulisha na dini mbali mbali kulingana na utafiti uliofanywa na Pew.
Mkuu wa wanachama hao nchini Kenya AIK, Harrison Mumia amemshtumu afisa wa usajili Maria Nyariki kwa kuendesha afisi yake kwa kukisia,na kwamba hajui athari za usajili wa kundi hilo.
Ameongezea kuwa kuna viongozi wa makanisa ambao wamewabaka watoto wadogo ,na wameruhusiwa kusajili makanisa yao.
AIK ina haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini Bw Mumia ameiambia BBC kwamba atawasilisha malalamishi hayo katika mahakama, kwa kuwa haki yao ya uhuru wa kushiriki imekiukwa.

AIK inaamini kwamba utambulizi rasmi wa kundi hilo utaliwezesha kushiriki zaidi katika maswala ya uma,mbali na kuliwezesha kufanya vitu kama vile kufungua akaunti za benki. Bwana Mumia amesema kuwa kama watu wasio amini kwamba Mungu yupo katika jamii ya kidini,yeye binafsi amebaguliwa. Mwaka uliopita AIK ilifeli katika jaribio la mahakamani kubatilisha uamuzi wa serikali kuwa na siku kuu ambayo itakayoambatana na siku ya ziara ya papa Francis nchini Kenya.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!