Wednesday, 3 February 2016

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NSSF YABORESHA HUDUMA ZAKE

Na. Lilian Lundo – Maelezo
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imejizatiti katika kuhakikisha kuwa utoaji  wa huduma kwa wateja wake zinakidhi  kiwango cha kimatiafa  ifikapo  mwaka 2020.

Hayo yalisemwa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Masoko NSSF Eunice Chiume alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya mabadiliko ya mifumo ili kuboresha utoaji huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko huo.“Miaka miwili iliyopita NSSF ilikuwa na mapungufu mengi kuliko ubora ambao ulipelekea NSSF kuboresha mifumo ya huduma zake na kufanikiwa kupata Tuzo ya utoaji bora wa
huduma mwaka 2014 iliyotolewa na British Standars Institute (BSI),” alisema Chiume.Chiume alitaja maboresho yaliyofanyika kuwa ni pamoja na mfumo mpya wa kupokea malalamiko ya wanachama ambapo kwa sasa malalamiko yanapokelewa na kutatuliwa kwa haraka tofauti na ilivyokuwa awali.
Katika mfumo huo mpya unamuwezesha mlalamikaji kutoa taarifa za kutoridhika na huduma kwa viongozi wakubwa wa NSSF kama vile meneja kiongozi masoko na uhusiano na mkurugenzi mkuu  ikiwa malalamiko yake hayajafanyiwa kazi ndani ya muda uliopangwa.
Chiume aliongeza kuwa maboresho mengine yamefanyika kwenye uchukuaji wa michango kwa mwanachama tofauti na awali ambapo  mwanachama alitakiwa kuonyesha barua kutoka kwa mwajiri wake ndipo mchakato wa malipo ufanyike  lakini kwa sasa NSSF huendelea na mchakato wa malipo  kwanza huku barua ikifanyiwa kazi.
Anaendela kubainisha kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na changamoto ya waajiri kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa  mwanachama hivyo NSSF iliamua kubadirisha mfumo huo, huku barua toka kwa mwajiri ikiendelewa kufuatiliwa.
NSSF pia imefungua kituo cha huduma kwa wateja pamoja na akaunti katika mitandao ya kijamii kama vile facebook na twitter ili wanachama na wadau wa NSSF waweze kutoa maoni au ushauri na kuwaondolea watu kero ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!