Mwanamuziki nyota nchini Vanessa Mdee,(kulia), akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa kongamano la wanachuo wa kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara, (UDBS), na kufanyika chuoni hapo ambapo Vanesa alikuwa ni mmoja wa watu waliotoa ushuhuda wa jinsi ya kutumia kipaji kama njia mojawapo ya kupata ajira licha ya kuwa na shahada ya sheria. Kushoto ni Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa Hiari PSS wa PSPF, Mwanjaa Sembe.
Afisa Masoko mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magire Werema, (kushoto), akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo na faida mbalimbali ambazo mwanachama anaweza kuzipata wakati wa kongamano la kutambua fursa lililowaleta pamoja wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu Cha Tumaini (tawi la Dar es Salaam). Magire aliwaambia wanafunzi hao kuwa wanachama wa PSPF ni pamoja na Watumishi wa sekta ya Umma, Binafsi, na watu wote walio katika Sekta isiyo Rasmi, (Wajasiriamali). Na kwamba Mwanachama anaweza kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko kama vile mikopo ya elimu, bima ya afya, fao la uzazi, mikopo ya nyumba na viwanja na lile la jipange kimaisha.
Mwanamuziki nyota nchini Vanes Mdee, akiweka dole gumba tayari kuchapa kwenye fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa kongamano lililowakusanya wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara na kufanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na mpango huo baada ya kupata elimu ya faida za kujiunga na mpango huo. Wanaoshuhudia, kutoka kulia ni Balozi wa PSPF, Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS wa Mfuko huo, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Rahma Ngassa.
Afisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gasper Lyimo, akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo, wakati wa kongamano lililowaleta pamoja wanafunzi wanawake wa mwaka wa mwisho wa chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Shule ya Biashara-UDBS), na kufanyika chuoni hapo
Balozi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Mrisho Mpoto, (kulia), akitoa “darasa” kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu Cha Tumaini (tawi la Dar es Salaam), kuhusu huduma na kazi zifanywazo na Mfuko huo wakati wa kongamano hilo
Anthony Luvanda, mhamasishaji kutoka kampuni ya Home of Events, akitoa mada juu ya changamoto za ajira na jinsi ya kuzikabili wakati wa kongamano lililowaleta pamoja wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu Cha Tumaini, (tawi la Dar es Salaam), lililoongozwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Rahma Ngassa, (aliyesimama), akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu Cha Tumaini, (tawi la Dar es Salaam), wakati wa kongamano la kujifunza kazi na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF. Rahma aliwataka wanafunzi hao kujiunga na PSPF ili kujiwekea mazingira mazuri ya maisha yao . Kulia ni Anthony Luvanda, na kushoto ni Magire Werema
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Hadji K.Jamadary (kushoto) na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo, Albert M.Feruzi, wakitoa “darasa” kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Shule ya Biashara), wakati wa kongamano la Wanawake wanachuo wa chuo hicho lililofanyika chuoni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa PSPF, Flaviana Matata
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard, akizungumza kwenye kongamano la wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Tumaini (tawi la Dar es salaam)
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akimpiga picha mwanafunzi huyu wa UDSM, tayari kwa kitambulisho huku wenzake wakisubiri huduma hiyo baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akizungumza kwenye kongamano la wanafunzi wanawake wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Shule ya Biashara), chuoni hapo. Kushoto ni Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata
Mpeperushaji wa vipindi vya wanawake kwenye runinga, Joyce Kiria, (kushoto), akielekzwa namna ya kujaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchagiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, na Balozi wa Mfuko huo, Flaviana Matata
Balozi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata, akiwaeleza wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Shule ya Biashara), jinsi ya kutumia vipaji vyao katika kujitengenezea ajira ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa PSPF.
Mwanafunzi huyu akimuuliza mwenzake wakati wanajaza fomu za kujiunga na PSPF kupitia mpango wa PSS
Afisa wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Hadji K. Jamadary, akiwa amezungukwa na wanafunzi wenye shauku wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaa, (Shule ya Biashara), baada ya kujiunga na Mfuko huo
Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, akiwa amezungukwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (shule ya biashara), mwishoni mwa kongamano hilo
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, “umevuna” mamia ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Shule ya Biashara), ambao wamejiunga ma mpango wa uchangiaji wa hiari PSPF Supplementary Scheme-PSS wakati wa kongamano lililopewa jina, (Women University Platform), na kufanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Sio tu wanafunzi pekee walijiunga na mpango huo, lakini pia watu maarufu kama vile, Mwanamuziki nyota wa muziki wa Bongo Flava, Vanessa Mdee,na mpeperushaji wa vipindi vya runinga vinavyohusu masuala ya wanawake, Joyce Kiria ambao walikuwa ni miongoni mwa wasemaji wakuu kwenye kongamano hilo walijiunga pia.
Kujiunga kwa wanafunzi hao kwenye mpango wa PSS, kulifuatiwa na mfululizo wa elimu ya huduma zitolewazo na Mfuko huo yaliyotolewa na Afisa a Operesheni wa PSPF, Hadji Jamadary, afisa matekelezo, Albert Feruzi, wakiongozwa na Meneja wa mpango huo, yaani PSS, Mwanjaa Sembe, na Balzoi wa PSPF, Mwnaamitindo “nguli” wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata.
Maafisa wa Mfuko huo, Rahma Ngassa, Gasper Lyimo na wengineo, walilazimika kufanya kazi ya ziada, kuwasaidia wanafunzi hao kujaza fomu hizo na kuchukua picha zao tayari kuwatengenezea vitambulisho.
Mambo yaliyowavutia wanafunzi hao na kuamua kujiunga na mpango huo ni zile faida wanazopata wanachama wa PSPF, kama vile Fao la mikopo ya elimu, jipange kimaisha, fao la uzazi, afya, na mikopo ya nyumba na viwanja.
Kongamano hilo lilitanguliwa na kongamano kama hilo lililofanyika Chuo Kikuu Cha Tumaini (tawi la Dar es Salaam, ambapo kazi kama hiyo ilifaywa na Mhamasishaji Anthony Luvanda, kutoka kampuni ya Home of Events, Afisa Masoko Mwandamizi, wa PSPF, Magire Werema, Rahma Ngassa, Delphin Richard, Gasper Lyimo na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto
No comments:
Post a Comment