Monday, 1 February 2016

MWILI WA MTANDANIA ULIOKWAMA INDIA KWA DENI LA MATIBABU WAWASILI LEO


Hatimaye mwili wa Mtanzania Abel Machanga aliyefia nchini India akipata matibabu unatarajiwa kuwasili leo baada ya kuzuiwa kwa takribani siku 28 kutokana na deni la matibabu.

Mwili huo umeruhusiwa baada ya familia ya Machanga kulipa deni la shilingi milioni 35 lililokuwa likidaiwa kama gharama za matibabu.

Abel alikutwa na mauti Desemba 31, 2015 akiwa kwenye matibabu nchini humo, mbaya zaidi, maiti yake ilizuiliwa kutolewa mochwari mpaka familia ilipe deni la shilingi milioni 35.
Abel alianza kuugua Novemba 2014 akiwa denti wa Chuo cha Biashara Dar (CBE). Alivimba macho, yakatokeza nje, akapoteza uwezo wa kuona huku pia akipumua kwa shida.


Alitibiwa Hospitali ya Macho CCBRT, Dar ikashindikana, akapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, hali ilizidi kuwa mbaya. Novemba 24, 2015, ndugu wakampeleka India ambapo mauti yalimkuta.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!