Wednesday, 3 February 2016
Mlipuko wa maambukizi ya Zika virus; Tanzania yatajwa
Kwa mujibu wa taarifa za shirika la "Centers for Disease Control and Prevention (CDC)",
(Areas with Zika | Zika virus | CDC), Tanzania ni moja ya nchi inayofahamika kuwahi kuwa na maambukizi ya Zika virus miaka ya nyuma (kabla ya 2015). Hii inatoa tahadhari kuwa katika maambukizi yanayoripitiwa duniani kwa sasa, Tanzania inaweza kuwa mhanga hasa ikizingatiwa kuwa Mbu wa Aedes wanaoeneza ugonjwa huo wamesambaa sehemu mbalimbali nchini.
Zika virus imekuwa gumzo kubwa duniani kwa sasa hasa kutokana na tatizo la watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya kutokukua vizuri kwa ubongo (microcephaly). Zaidi ya watoto 4000 waliozaliwa 2015 wameripotiwa kuathirika nchini Brazili huku wengine zaidi ya 3500 wakiendelea kuchunguzwa. Watoto wanazozaliwa na microcephaly huwa na mtindio wa ubongo lakini visa vichache vya vifo kwa watoto hao pia hutokea.
Hata hivyo kwa sasa maambukizi active yapo zaidi katika nchi za karibean na Ocenia (Samoa).
Katika maambukizi yanayotokea sasa, hadi kufikia jana mgonjwa mmoja alikuwa amethibitishwa kupata ugonjwa huo nchini Marekani na wawili Australia. Pia kumekuwa na matukio machahce yaliyoripotiwa nchini Thailand.
Kama maambikizi ya Zika virus yapo sasa ama la kwa nchi yetu bado ni kitendawili kwani uwezo wa taasisi za afya kuchunguza na kuthibitsha magonjwa ya virus unajulikana kuwa mdogo.
Ikumbukwe kwamba maambuki zi Zika virus husababisha tu homa kidogo, macho kuwasha, kichwa kuuma, na maumivu ya viungo. Hizi ni dalili "za kawaida" sana katika jamii yetu ambazo kwa kiasi kikubwa huchukuliwa kama malaria na watu wengi hujitibu malaria wanapoona dalili hizi.
Lakini pia ikumbukwe kuwa maambukizi ya Zika virus husababisha dalili kwa watu wachache, huku wengi yakipita bila kuonyesha dalili zozote.
Tatizo kubwa la Zika virus ambalo limeshuhudiwa sasa ni athari kwa watoto walipata maambukizo wakiwa tumboni kwa mama zao kama ilivyoelezwa hapo juu.
Naamini serikali imejipanga katika mikakati ya kupambana na tatizo hili linalotoa changamoto kubwa kwa sekta ya afya duniani, na naamini kujenga "public awareness" ni hatua muhimu ya awali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment