Saturday 6 February 2016

LIKUVI: WALIOSHINDWA KUENDELEZA MASHAMBA WAJISALIMISHE


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amekerwa na kodi ndogo wanayolipa wawekezaji wilayani hapa na kuagiza wanaoshindwa kuyaendeleza mashamba wasalimishe hati za mashamba hayo.

Alitoa agizo hilo mjini hapa juzi wakati akizumza na mwekezaji wa Ranchi ya Darakuta, Raphael Baptist.
“Natoa onyo kwa wawekezaji waliopewa mashamba na wakashindwa kuyaendeleza wasalimishe hati zao, wawekezaji tunategemea waanze na mtaji wao na sio kwenda kukopa benki kwa kutumia mashamba wanayopewa,” alisema.
Pia aliwataka wawekezaji waliouza ardhi waliyopewa kwa wawekezaji wengine wasalimishe hati zao na serikali itazifuta.
Kwa upande wake, mwekezaji wa ranchi hiyo alisema alinunua ardhi yenye ukubwa wa hekari 32,000 lakini kwa sasa anazozitumia ni 1,7500 kwa ajili ya kufuga ng’ombe, kulima miwa na kupanda miti tangu mwaka 1985 alipopewa rasmi na serikali.
“Mwaka 1985 nimlinunua shamba hili kwa Sh. milioni 8.4 za Tanzania na faida ninazopata ni kufuga na kulipa kodi Mamlaka ya Mapato (TRA) na kuwalipa watumishi 80 niliowaajiri,” alisema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!