Friday, 19 February 2016

FAHAMU MADHARA YA SUKARI MWILINI



Wengi hutumia sukari mara kwa mara kwenye chai,juisi,soda,keki,pipi nk kwani sukari ni chakula halali tena kitamu sana.Japo kinapendwa sana lakini kinaangukia katika kundi la vyakula ambavyo siyo vizuri endapo itatumiwa kiholela.



.Sukari ina madhara mengi kama kuzeesha haraka na kujenga mazingira ya kurahisisha kupatwa na magonjwa ya kimfumo kama vile jongo'Gout',shinikizo la damu,matatizo ya moyo na saratani. Sukari inazeesha kwa molecule zake kun'gan'gania kwenye protini za seli katika mchakato ambao kitaalamu huitwa'Glycation',un'gan'ganizi husababisha kuzalishwa kwa chembechembe ambazo husababisha kukakamaa kwa tishu na kupoteza maumbile yake asili na kwa nje hujitokeza kama makunyanzi kwenye ngozi na kupauka na kwa wenye ugonjwa wa kisukari ambao mzunguko wao wa damu hukaa na kiwango kikubwa cha sukari muda mwingi,madhara ya ziada ni uharibifu wa mishipa midogo ya damu kwenye macho na ile inayopeleka damu kwenye neva

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!