Eczema(atopic dermatitis) ni ugonjwa wa ngozi ,unaofanya ngozi kuwasha sana kuwa kavu na kupata vijipele vidogo vidogo vyenye rangi nyekundu,huu ugonjwa ushambulia watoto na wakubwa sehemu za viungo vya mwili (joints) mkononi
Shingoni na miguuni na inaweza tokezea sehemu ya usoni ,juu ya jicho ,makwapani,mgongoni ,tumboni ,mbele ya kichwa (forehead),mapajani,mdomoni na mashavuni. Watoto walio chini ya miaka 5 huwa adhiri kwa asilimia 15% unaweza chukua mda kupona kulingana na ngozi na kiasi cha mtoto alivyoadhirika.
Chanzo cha ugonjwa wa eczema
Eczema inasababishwa na mwili kushindwa kutengeneza au kuzalisha ceramider ,ceramider ni fatty cell inayotumika kwenye uzalishwaji wa ngozi,ceramider inaposhindwa kuzalishwa ngozi ya mtoto inapoteza kiwango cha maji na kuifanya kuwa kavu na ndipo inapomso sababishia kuanza kujikuna ,ngozi kuwa kavu na kubadilika rangi kuwa nyekundu.
Eczema ni ugonjwa wa kuridhi -toka kwa mama / baba aliekuwa na ugonjwa ni rahisi mtoto akaridhi.
Mzingo(Allergy au asthma)na pumu huleta eczema
Nini kinachochea kutopona eczema haraka kwa mtoto
Mtoto mwenye tatizo la eczema anatakiwa aepushwe
Ngozi kuwa kavu (dry skin)-epuka ngozi ya mtoto kuwa kavu itasababisha kuwa na low humidity na kujikuna sana .
Joto kali-joto linapokuwa kali inamsababisha mtoto kujikuna zaidi ,usimveshe mtoto nguo nyingi kipindi cha joto itamfanya ajikune sana .
Food allergy-kuna baadhi ya vyakula vyenye kuleta allergy inatakiwa asipewe kama maziwa,mtindi,mayai,cheese ,nuts(karanga,korosho nk)mikate,pweza,kamba
Acid fruits-matunda yen acid asitumie ndimu ,machungwa,nyanya,strawbell
Acha kutumia vitu vya harufu kali kama sabuni ,perfumes ,majani,na mafuta
Kuogeshwa kwa mda mrefu-epuka kumwogesha kwa mda mrefu au kukaa ndani ya maji isizidi dakika 10 maji yana sababisha ngozi kuwa kavu zaidi,atumie maji vugu vugu wakati wa kumwogesha tumia sabuni ya (sensitive skin) isiyo na harufu na usitumie shampoo
Nguo za kumbana-usimveshe nguo za kumbana au zenye matrial ya synthetic fabric, wool, ,mveshe nguo za kupwaya ziwe material ya cotton inamfanya ajisikie vizuri bila miwasho.
Nguo mpya-nguo mpya inamfanya ajikune zaidi ,kabla ujamvesha fua kwanza.
Sabuni ya kufulia nguo -nayo inaweza msabishia kuwashwa zaidi ,fatilia kila ufuapo kama ukimvesha izo nguo na kuwashwa sana ujue iyo sabuni haimfai
Kucha kuwa ndefu-zitamkwarua na kujikuna sana kuharibu ngozi zaidi ,hakikisha kucha zake ni fupi kila mara.
Tiba
Eczema kutibika kwa haraka ni ngumu ,kuna dawa za kupaka na ikapunguza muwasho, fatilia masharti hayo nilioandika hapo juu na kula matunda na mboga mboga kwa wingi
yanayoweza tibu au punguza eczema kwa kiasi kama parachichi ,ndizi mbivu, papai,apple,juice ya carrots ,tango,aloe vera,spinanch ,viazi vitamu,viazi ulaya,smoothie ya tango,parsley,broccoli na tangawizi kidogo saga pamoja wapewe kwa watoto walio juu ya miezi 6 ,samaki wa maji baridi kama salmon wanafaa zaidi wana omega 3 ya kutosha.Mwepushe mtoto kula fast food zinachochea ugonjwa kuongezeka.
Eczema inaweza itachukua mda mtoto kupona akuavyo ndivyo ugonjwa unapotea.Utakapo ona mtoto wako ana dalili ya eczema mpeleke kwa pediatriacian au dermatolost atampima na atamwandikia antiobioc na cream za kutumia kupunguza kujikuna.
Mpake kimoja wapo kati ya hivi mafuta ya nazi ,lotion, ointments au creams mara kwa mara unapo ngozi yake ipo kavu,akitoka kuoga usichelewe kupaka mafuta
Mveshe mtoto nguo ya mkono mrefu usiku akitaka kulala ili asijikune
Mwepushe kumpa vyakula vya kukaangwa
Asile vyakula vyenye spices(viungo) ukipika chakula cha familia tenga mboga yake kabla ujaweka spices.
Home remedies
Unaweza kutengeneza dawa ya eczema kwa kutumia vitu asilia
Mahitaji
vijiko 3 vya extra virgin olive oil
kijiko kimoja cha baking soda
vijiko 2 vya oats iliosagwa
Jinsi ya kuandaa
Weka maji kwenye beseni au ndoo changanya na huo mchanganyiko koroga wacha huo mchanganyiko kwa dakika 15-20 ndio aogee
inamsaidia ngozi kuwa ng’aavu na laini itaondoa ile hali ya kujikuna.
Dawa nzuri za eczema – Aveeno baby,Eucerin,proecza,,Aquaphor,cetaphir,Dermatex,Diprobase,Ezerra na nyinginezo onana na daktari wa watoto kabla ujanunua dawa na atakapo tumia uwe mvulimivu sio kitu cha kupona haraka ila mabadiliko utayaona kwa mda mfupi tu.
SHUKRANI KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO
No comments:
Post a Comment