Rorya. Mkazi mmoja wa Rorya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake na kumwambukiza Virusi vya Ukimwi (VVU).
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Wilaya, Sweetbert Njewike alisema mtoto huyo ana miaka 12 na anasoma Shule ya Msingi ya Nyarombo.
Nyewike alisema baada ya jeshi hilo kupata taarifa, lilimkamata mtu huyo, (jina tunalihifadhi hadi atakapofikishwa kortini) na walimfanyia vipimo vya afya ili kujiridhisha na tuhuma kuwa mtuhumiwa pia anaishi na VVU kwa zaidi ya miaka tisa.
“Taarifa zilizofika katika ofisi zetu zilisema mtuhumiwa alikuwa amemrithi bibi wa mtoto huyo baada ya kufiwa na mume wake aliyekufa kwa Ukimwi, hivyo na mrithi wake ni lazima atakuwa mgonjwa na atakuwa amemuambukiza mtoto huyo,” alisema Nyewike.
Nyawike alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akifanya tendo la ndoa na mtoto huyo tangu Februari 2015 akiwa darasa la tatu na wote kwa pamoja walipimwa na kukutwa wakiwa na maambukizi ya VVU.
Mmoja wa wataalamu wa maabara katika Hospitali ya Shirati (KMT), Richard Kaira alithibitisha mtoto huyo kupimwa na kubainika kuwa na maambukizi hayo.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Macktrida Charles alisema alipokea malalamiko kutoka kwa mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo na alimshauri kwenda kutoa taarifa polisi na kupima afya.
“Wilaya hii imekithiri kwa kesi za ubakaji. Mwaka jana tulikuwa na kesi zaidi ya 30 na hutokea ndani ya familia, hivyo ni vigumu kuzidhibiti kwa kuwa huzimaliza katika vikao vya ukoo bila kutushirikisha,” alisema Charles.
Mama mzazi wa binti huyo, Veronica Thindo alisema baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake ana uhusiano wa kimapenzi na babu yake ambaye ni mrithi wa bibi yake, alishtuka na kuchukua vipimo ili kuhakikisha kama atakuwa salama kwa kuwa alikuwa akifahamu afya ya mama mkwe wake si salama.
No comments:
Post a Comment