Tuesday 23 February 2016

AJALI:

 Basi la Nata Raha lagonga nyumba na kusababisha vifo vya watu saba huko Bunda leo, Mganga Mkuu Nicholas Machochota athibitisha. 4 wakimbizwa Bugando, Mwanza.


Watu saba wamafariki wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la nata raha yenye namba za usajili T 473 CJN linalofanya safari zake kati ya Mugumu wilayani serengeti kupitia Bunda kwenda mkoani Mara kupalamia nyumba eneo   la njia nne mjini Bunda baada ya breki za basi hilo kukatika likiwa katika mteremko mkali. 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bunda, akizungumza baada ya kufika eneo la tukio, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa tano asbuhi na kusema kati ya majeruhi hao wanane wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza huku wengine wakilazwa hospitali teule ya DDH mjini Bunda.
 
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamedai baada ya kukaribia njia kuu   ya Mwanza Musoma mita chache tu kufika kituo kikuu cha mabasi mjiniBunda mwendo wa basi hilo uliongezeka na baada ya kuhoji walielezwa kuhusu kukatika kwa breki hizo kabla ya kuvamia jengo hilo.
 

Hata hivyo wakati mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama akisema walifariki ni abiria saba lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mara ACP Philip  Alex Kalangi akizungumza na ITV kwa njia ya simu  amesema abiria sita ndiyo waliofariki katika ajali hiyo.



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!