Wazazi
na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule
ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba
Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa
elimu bure nchini.
Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya
kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha
Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani
wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.
Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa
tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo
hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.
Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari
kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo
lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu
ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu
Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi
ruzuku kwa ajili yao.
Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma
Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.
Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa
wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao
kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.
Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya
Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi
waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100
kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango
mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa
mwaka.
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group
No comments:
Post a Comment